Thursday, 15 February 2018

NAPENDA BIASHARA

BIASHARA NZURI KUFANYA KWA MWAKA 2018

Kutokana na serikali kubana matumizi na kusababisha pesa kupungua katika mzunguko, watu wengi hususani Wenye mitaji midogo wamebaki hawajui ni biashara gani wafanye yenye kuhitaji mtaji kidogo lakini iwe na faida nzuri.
        Hali hii imekuwa kikwazo kwa wengi wanaotamani kuanzisha biashara hasa wale wasiofuatilia mafunzo ya biashara na ujasirimali na elimu ya fedha kwa ujumla.
         Leo nitakushirikisha kwa ufupi biashara chache na uwekezaji unaoweza kufanya kipindi hiki cha uadimu wa pesa.
          Zifuatazo ni biashara tatu zinazohitaji mtaji kidogo lakini zinafaida kubwa kwa sana:-
 
     1)Biashara yya kuuza chakula (mgahawa). Hata Kama pesa imekuwa adimu vipi watu lazima wale, jaribu kufanya utafiti aina ya chakula kinachohitajika sana katika eneo lako kisha anza biashara hiyo mara moja.

        (2)Kilimo cha kibiashara. Kilimo hiki kinahusisha mazao pendwa ambayo hukomaa ndani ya muda mfupi hasa mazao ya bustani na matunda.
   
        (3)Ufugaji wa kibiashara. Ufugaji huu unahusisha wanyama Kama sungura, ng'ombe wa maziwa pamoja na kuku.

        Uwekezaji ambao unaweza kufanya usiohitaji muda wako mwingi kuusimamia.
        
           (1)Uwekezaji katika mfuko wa umoja wa UTT, tembelea ofisi zao kupata maelezo mhimu.
            (2)Kununua hisa katika soko la hisa.  hapa unatakiwa uwe unafuatilia kwa makini ili kujua soko la hisa likoje na kampuni gani hisa zake zinauzika kirahisi kwa faida.
             (3)Biashara ya mtandao (network marketing).Biashara hii inahitaji umakini na elimu ya kutosha juu ya biashara hii, nakushauri upate kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO kilichoandikwa na Amani makrita, Tsh 5000 unapata soft copy wasiliane naye kwa namba 0755953887
             (4)Uwekezaji katika viwanja. Nunua kiwanja na kiache tu baada ya muda utauza kwa faida.
           (5)Wekeza katika majengo. Kama una mtaji wa kutosha jenga nyumba aidha ya kuishi au kibiashara halafu pangisha.

MHIMU:- Kuna changamoto kubwa ya baadhi ya watu kuwa na mtaji lakini wanashindwa kuanza biashara kwa sababu ya kukosa muda wa kusimamia biashara hizo. Suluhu ya changamoto hii ni kutafuta MSHIRIKA.
        Mshirika wako katika biashara si mfanyakazi wako bali ni mtu ambaye kwa pamoja mnamiliki biashara hiyo.

    Faida ya kuwa na mshirika
(1)Ataweza kufuatilia mambo mhimu ya biashara ambayo wewe huwezi kufuatilia kutokana na kubanwa na kazi.
(2)Kama kazi yako hairuhusu kuwa na biashara unaweza kuanza biashara kwa njia hii.

       Mambo ya kuzingatia kwa mtu unaye mchagua kuwa mshirika wako.
(1)Uaminifu
(2)Kujituma kwenye kazi
(3)Awe na malengo na nidhamu ya fedha
(4)Asiwe na tabia hatarishi Kama ulevi na starehe.
(5)Awe na uelewa juu ya biashara mnayo taka kufanya.

     
                            Chief Mwinula

Sunday, 14 January 2018

ZAMA ZA HABARI

                  ZAMA ZA SASA
      Baada ya Zama za viwanda (industrial age) kupita sasa tupo katika zama za habari (information age). Enzi ya Zama za viwanda kulikuwa na kauli mbiu ya SOMA KWA BIDII PATA MAKISI NZURI PATA AJILI  NZURI ISHI MAISHA MAZURI. Katika zama hizo mfanyakazi Pekee ndiye aliyekuwa na usalama wa maisha yake kiuchumi (job security). Lakini kauli mbiu katika zama hizi za sasa ni MWENYE HABARI SAHIHI KWA MUDA SAHIHI NDIYE ANAYEFANIKIWA. Haitoshi tu kuwa na habari sahihi ukafanikiwa bali pia yakupasa kuwa na MAARIFA SAHIHI.
      Naposema maarifa sahihi simanishi uhalali wa taaluma yako, bali ni maarifa ya ziada ambayo yanaweza kuibadilisha hiyo habari sahihi na kuwa pesa. Kwa lugha nyingine hiyo habari sahihi ni FURSA.
        Fursa inaweza ikawa imeenda sambamba na taaluma yako, au inaweza ikahusika na eneo unaloishi, au ikawa sawa na kazi unayofanya, na pengine ikawiana na muda wako wa ziada. Lakini ikawa ngumu kwako kuitumia kwa sababu huna maarifa ya ziada hivyo ukashindwa kunufaika nayo.
          Hivyo basi katika zama hizi za habari kuna elimu ambazo hutakiwi kuzikosa hata kidogo angalau kila siku ya maisha yako kwani utaongeza maarifa ya ziada ili uweze kukabiliana vyema na fursa zinazojitokeza. Elimu hizi ni kama ifuatavyo:-
      (1)ELIMU YA PESA, hii itakusaidia kuielewa pesa kwa undani zaidi inavyopatikana, inavyopaswa kutumika, inavyoweza kuongezeka na miiko yake. Kwa ujumla uelewe kanuni ya pesa, kwani wengi hushindwa kutumia fursa kwa kisingizio cha kukosa pesa.
        (2)ELIMU YA BIASHARA NA UJASILIAMALI, hii itakusaidia kuelewa kanuni ya kuanza kidogokidogo kufikia mafanikio, namna ya kukuza biashara, jinsi  ya kuepuka hatari katika biashara, utajifunza kanuni za mauzo na ushindani pia utajifunza uthubutu. Watu wengi wanashindwa kuanza biashara kwa kukosa maarifa ya uthubutu pia biashara nyingi hufa mapema kwa kukosa maarifa haya.
      (3)ELIMU YA MAHUSIANO, hapa namaanisha uhusiano baina yako na jamii inayokuzunguka, Kama vile ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzio na kila mtu unayekutana naye haijalishi mnafahamiana au laa. Hii itakuweka karibu na kila mtu hivyo utajiongezea wigo wa kupata habari nzuri za fursa, na pengine kupata mtu mwenye uwezo wa kukupa sapoti kimawazo na kifedha pia.
         (4)ELIMU YA TEKINOLOJIA NA MAWASILIANO, hii itakusaidia kupata habari mapema kupitia vyombo vya kisasa vya mawasiliano Kama vile simu na komputa kupitia internet. Pia itakurahisishia utekelezaji wa fursa zako Kama vile online marketing, electronic business(biashara mtandaoni)  pamoja na  kupata ujuzi zaidi wa kitu unachofanya kupitia maandiko na video za mtandaoni.
  
        Asilimia kubwa elimu hizi hazimo kwenye mitaala ya mfumo wetu rasmi wa elimu nchini, hata Kama baadhi zipo lakini si katika mkitadha wa kile ninachokimaanisha cha ulazima wa kila apendaye mafanikio ajifunze maarifa haya haijalishi ana taaluma gani.
            Maarifa haya unaweza kuyapata kwa kusoma vitabu kuhudhuria semina, kusikiliza mafundisho kwa njia ya sauti(audio) au video mtandaoni pia kwa kupata ushauri na uzoefu kwa wale walioanza zamani kuyaishi maarifa haya.
  NB, ukishayapata maarifa haya, anza kuyafanyia kazi Mara moja ndipo utakapoona ilivyo rahisi kufanikiwa katika Zama hizi za habari.
                     ASANTE
           Tumia fursa yako
             Chief Mwinula