Thursday, 15 February 2018

NAPENDA BIASHARA

BIASHARA NZURI KUFANYA KWA MWAKA 2018

Kutokana na serikali kubana matumizi na kusababisha pesa kupungua katika mzunguko, watu wengi hususani Wenye mitaji midogo wamebaki hawajui ni biashara gani wafanye yenye kuhitaji mtaji kidogo lakini iwe na faida nzuri.
        Hali hii imekuwa kikwazo kwa wengi wanaotamani kuanzisha biashara hasa wale wasiofuatilia mafunzo ya biashara na ujasirimali na elimu ya fedha kwa ujumla.
         Leo nitakushirikisha kwa ufupi biashara chache na uwekezaji unaoweza kufanya kipindi hiki cha uadimu wa pesa.
          Zifuatazo ni biashara tatu zinazohitaji mtaji kidogo lakini zinafaida kubwa kwa sana:-
 
     1)Biashara yya kuuza chakula (mgahawa). Hata Kama pesa imekuwa adimu vipi watu lazima wale, jaribu kufanya utafiti aina ya chakula kinachohitajika sana katika eneo lako kisha anza biashara hiyo mara moja.

        (2)Kilimo cha kibiashara. Kilimo hiki kinahusisha mazao pendwa ambayo hukomaa ndani ya muda mfupi hasa mazao ya bustani na matunda.
   
        (3)Ufugaji wa kibiashara. Ufugaji huu unahusisha wanyama Kama sungura, ng'ombe wa maziwa pamoja na kuku.

        Uwekezaji ambao unaweza kufanya usiohitaji muda wako mwingi kuusimamia.
        
           (1)Uwekezaji katika mfuko wa umoja wa UTT, tembelea ofisi zao kupata maelezo mhimu.
            (2)Kununua hisa katika soko la hisa.  hapa unatakiwa uwe unafuatilia kwa makini ili kujua soko la hisa likoje na kampuni gani hisa zake zinauzika kirahisi kwa faida.
             (3)Biashara ya mtandao (network marketing).Biashara hii inahitaji umakini na elimu ya kutosha juu ya biashara hii, nakushauri upate kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO kilichoandikwa na Amani makrita, Tsh 5000 unapata soft copy wasiliane naye kwa namba 0755953887
             (4)Uwekezaji katika viwanja. Nunua kiwanja na kiache tu baada ya muda utauza kwa faida.
           (5)Wekeza katika majengo. Kama una mtaji wa kutosha jenga nyumba aidha ya kuishi au kibiashara halafu pangisha.

MHIMU:- Kuna changamoto kubwa ya baadhi ya watu kuwa na mtaji lakini wanashindwa kuanza biashara kwa sababu ya kukosa muda wa kusimamia biashara hizo. Suluhu ya changamoto hii ni kutafuta MSHIRIKA.
        Mshirika wako katika biashara si mfanyakazi wako bali ni mtu ambaye kwa pamoja mnamiliki biashara hiyo.

    Faida ya kuwa na mshirika
(1)Ataweza kufuatilia mambo mhimu ya biashara ambayo wewe huwezi kufuatilia kutokana na kubanwa na kazi.
(2)Kama kazi yako hairuhusu kuwa na biashara unaweza kuanza biashara kwa njia hii.

       Mambo ya kuzingatia kwa mtu unaye mchagua kuwa mshirika wako.
(1)Uaminifu
(2)Kujituma kwenye kazi
(3)Awe na malengo na nidhamu ya fedha
(4)Asiwe na tabia hatarishi Kama ulevi na starehe.
(5)Awe na uelewa juu ya biashara mnayo taka kufanya.

     
                            Chief Mwinula

Sunday, 14 January 2018

ZAMA ZA HABARI

                  ZAMA ZA SASA
      Baada ya Zama za viwanda (industrial age) kupita sasa tupo katika zama za habari (information age). Enzi ya Zama za viwanda kulikuwa na kauli mbiu ya SOMA KWA BIDII PATA MAKISI NZURI PATA AJILI  NZURI ISHI MAISHA MAZURI. Katika zama hizo mfanyakazi Pekee ndiye aliyekuwa na usalama wa maisha yake kiuchumi (job security). Lakini kauli mbiu katika zama hizi za sasa ni MWENYE HABARI SAHIHI KWA MUDA SAHIHI NDIYE ANAYEFANIKIWA. Haitoshi tu kuwa na habari sahihi ukafanikiwa bali pia yakupasa kuwa na MAARIFA SAHIHI.
      Naposema maarifa sahihi simanishi uhalali wa taaluma yako, bali ni maarifa ya ziada ambayo yanaweza kuibadilisha hiyo habari sahihi na kuwa pesa. Kwa lugha nyingine hiyo habari sahihi ni FURSA.
        Fursa inaweza ikawa imeenda sambamba na taaluma yako, au inaweza ikahusika na eneo unaloishi, au ikawa sawa na kazi unayofanya, na pengine ikawiana na muda wako wa ziada. Lakini ikawa ngumu kwako kuitumia kwa sababu huna maarifa ya ziada hivyo ukashindwa kunufaika nayo.
          Hivyo basi katika zama hizi za habari kuna elimu ambazo hutakiwi kuzikosa hata kidogo angalau kila siku ya maisha yako kwani utaongeza maarifa ya ziada ili uweze kukabiliana vyema na fursa zinazojitokeza. Elimu hizi ni kama ifuatavyo:-
      (1)ELIMU YA PESA, hii itakusaidia kuielewa pesa kwa undani zaidi inavyopatikana, inavyopaswa kutumika, inavyoweza kuongezeka na miiko yake. Kwa ujumla uelewe kanuni ya pesa, kwani wengi hushindwa kutumia fursa kwa kisingizio cha kukosa pesa.
        (2)ELIMU YA BIASHARA NA UJASILIAMALI, hii itakusaidia kuelewa kanuni ya kuanza kidogokidogo kufikia mafanikio, namna ya kukuza biashara, jinsi  ya kuepuka hatari katika biashara, utajifunza kanuni za mauzo na ushindani pia utajifunza uthubutu. Watu wengi wanashindwa kuanza biashara kwa kukosa maarifa ya uthubutu pia biashara nyingi hufa mapema kwa kukosa maarifa haya.
      (3)ELIMU YA MAHUSIANO, hapa namaanisha uhusiano baina yako na jamii inayokuzunguka, Kama vile ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzio na kila mtu unayekutana naye haijalishi mnafahamiana au laa. Hii itakuweka karibu na kila mtu hivyo utajiongezea wigo wa kupata habari nzuri za fursa, na pengine kupata mtu mwenye uwezo wa kukupa sapoti kimawazo na kifedha pia.
         (4)ELIMU YA TEKINOLOJIA NA MAWASILIANO, hii itakusaidia kupata habari mapema kupitia vyombo vya kisasa vya mawasiliano Kama vile simu na komputa kupitia internet. Pia itakurahisishia utekelezaji wa fursa zako Kama vile online marketing, electronic business(biashara mtandaoni)  pamoja na  kupata ujuzi zaidi wa kitu unachofanya kupitia maandiko na video za mtandaoni.
  
        Asilimia kubwa elimu hizi hazimo kwenye mitaala ya mfumo wetu rasmi wa elimu nchini, hata Kama baadhi zipo lakini si katika mkitadha wa kile ninachokimaanisha cha ulazima wa kila apendaye mafanikio ajifunze maarifa haya haijalishi ana taaluma gani.
            Maarifa haya unaweza kuyapata kwa kusoma vitabu kuhudhuria semina, kusikiliza mafundisho kwa njia ya sauti(audio) au video mtandaoni pia kwa kupata ushauri na uzoefu kwa wale walioanza zamani kuyaishi maarifa haya.
  NB, ukishayapata maarifa haya, anza kuyafanyia kazi Mara moja ndipo utakapoona ilivyo rahisi kufanikiwa katika Zama hizi za habari.
                     ASANTE
           Tumia fursa yako
             Chief Mwinula

Friday, 29 December 2017

KIFUNGO CHA FIKRA

TAFAKURI YA MWISHO WA MWAKA 2017

AMUA KUWA HURU KUTOKA KATIKA KIFUNGO  CHAKO

Katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania tumeshuhudia Rais na Amiri Jeshi mkuu akitumia vyema wajibu wake wa kisheria kusamehe wafungwa kwa baadhi yao kuwaachia huru na wengine kuwapunguzia vifungo vyao.
Kikubwa zaidi kilichoibua shangwe, furaha na pengine mijadala kila kona ya nchi ni kitendo  cha Raisi kusamehe Wale waliokuwa wamefungwa kifungo cha maisha pamoja na baadhi ya Wale waliohukumiwa kunyongwa.
Kitendo cha mfungwa kuachiwa huru huleta furaha kubwa Sana kwake na kwa familia yake pia. Hii hutokana na ukweli kwamba hufufua ndoto na malengo yake ambayo ni dhahiri yalianza kupotea kutokana na kuwa katikati ya kuta za gereza pasipo na matumaini ya kutoka.  Hata kama mfungwa huyo alifungwa kifungo cha muda maalumu ndoto zake huchelewa kutimia kutokana na muda anaopoteza akiwa gerezani.

Msamaha kwa mfungwa hutokana na bahati tu kwani kwani kuna wafungwa wengi walio na nafasi ya kusamehewa kutokana na vigezo husika, lakini kutokana na ufinyu wa nafasi za msamaha ndipo Bahati ikamwangukia aliyesamehewa.
      Tukiacha wafungwa walio magerezani kwa sababu ya makosa mbalimbali kutokana na sheria na taratibu za nchi ambao wanapaswa kukaa humo kwa muda fulani, maisha au pengine kusubiria kunyongwa au kubahatika msamaha, pia kuna wafungwa wengi sana katika jamii yetu ambao kisheria wako huru lakini kifikra wamezungukwa na kuta nene za gereza huru.
        Wafungwa wa namna hii wapo wengi sana lakini kwa walio wengi hawajitambui kuwa wako kifungoni kwa kiburi cha kuwa huru kisheria. Kifungo cha namna hii ni cha fikra. Fikra zimefungwa na mambo mbalimbali ambayo kiukweli yanatesa sehemu kubwa ya maisha na pengine kusababisha majuto makubwa kwa mhusika. Jambo la heri ni kwamba vifungo vya namna hii havihitaji Msamaha kutoka kwa mtu/kiongozi yeyote bali ni uamuzi wa mhusika kuamua kuwa huru baada ya kukitambua kifungo chake.
       Katika makala hii nitajaribu kukupitisha katika sehemu mbalimbali za yetu ya kila Siku ambayo ni vifungo Lakini hatuvitambui. Kama utaweza kutambua kifungo moja wapo kinahusu maisha yako, amua mara moja kuchukua uamuzi wa busara kuwa huru.
        1)MADENI# Kuna watu wapo katika kifungo cha madeni, wamekopa na wanadaiwakkila kona ya mtaa mpaka imefikia hatua wanakosa raha na kujutia. Mbaya zaidi ni kwamba pesa walizokopa hazikufanya kazi kama walivyotarjia, hivyo wamebaki wakilipa madeni kwa Majuto. Mipango yao imesimama kupisha madeni.
           2)KIPATO KUTOKIDHI MAHITAJI# mtindo huu wa maisha unawatesa watu wengi Sana, wafanyakazi serikalini, sekta binafsi na Wale wenye shughuli zao binafsi. Wanapata kipato kutokana na aidha mishahara, au kutokana na shughuli zao zingne Kama bisahara lakini kipato hiki hakikidhi mahitaji au kushindwa kutimiza malengo yao mhimu. Hiki ni kifungo kibaya kuliko vyote na ndo chanzo kikuu cha vifungo vingine kama madeni, maagano ya kishetani, sonona (msongo wa mawazo), ulevi, na kwa asilimia kubwa kinaweza kusbabisha mtu kufanya maovu kinyume na sheria hatimaye kuangukia katika kifungo halisi cha gerezani.
        3) KUTEGEMEA MISAADA# kuna watu wanaendesha maisha yao kwa kuombaomba kutoka kwa ndugu, viongozi, waajiri wao, au Jamaa zao.Maisha ya namna hii yanakufanya ushindwe kuamua msitakabali mzima wa maisha yako kwani wanaokusaidia ndio wenye maamuzi juu ya ratiba yako, muda wako, na nguvu zako pia. achana na kifungo cha namna hii badala yake wekeza muda wako, nguvu zako, pamoja na mawazo yako kwenye  mipango na ndoto zako.
        4)ULEVI NA MADAWA YA KULEVYA# kutokujizuia katika ulevi ni kifungo. Majuto yake huonekana kutokana na madhara yatokanayo na matumizi ya pombe na madawa mengine ya kulevya. MFANO: kufirisika, ajali, ulemavu uliopata kutokana na ugomvi wa kilevi, pia maelewano duni katika familia yako sababu ya ulevi. Amua sasa kuachana na kifungo hiki.
         5)MFUMO WA MAISHA UNAOENDEKEZA NI KIFUNGO KWAKO# kuna baadhi ya mifumo ya maisha isiyo na faida imewafanya baadhi ya watu kuteseka kifikra pasipo sababu ya msingi. Pengine kupitia vitu fulani ambavyo wanapenda kuvitumia ambavyo siyo mhimu lakini huwafanya wateseke wakivikosa. Mfano:- sigara, kahawa, kucheza karata, bao au hata kuangalia kipindi fulani cha televisheni. Amua sasa kupunguza ama kuachana kabisa na m
Vitu hivi na utumie muda na akili yako kukamilisha ndoto zako.
         6)MATUMIZI YA MITANDAO  YA KIJAMII# Ni dhahiri kuwa kila maendeleo huja na kasoro zake, kukua kwa teknolojia ya mawasiliano hasa ujio wa simu Za smartphone na uanzishwaji wa mitandao kama facebook, whatsapp, twitter na mingine mingi imekuwa tatizo kwa watumiaji  kwani
       Walio wengi wanapoteza muda wao mwingi kwenye mitandao kwa mambo ya ovyo kabisa. Watumiaji wa namna hii huteseka Sana kimawazo wakikosa pesa ya kununulia kifurushi cha internet. Kama nawe ni miongoni mwao,yakupasa uwe huru kwa kutumia vizuri teknolojia hii.
       🐇  NB: MICHEZO YA KUBAHATISHA NAHISI NAYO NI KIFUNGO HURU KIPYA ZAIDI  😃

Tunapofunga mwaka 2017 achana na mifumo ya maisha yako ambayo kupitia makala hii umetambua kuwa ni kifungo kwako. Achana na yale yaliyokukwamilisha kufikia malengo yako pasipo sababu za msingi.
                          "Tawala maisha yako"
              Chief Mwinula

Sunday, 24 September 2017

BIASHARA

ANZISHA BIASHARA YAKO SASA

            sehemu ya kwanza

1.Kuanzisha biashara ni moja ya maamuzi mazuri na sahihi katika maisha. Lakini ukianza bila Elimu ya kutosha juu ya biashara hiyo itakuwa kazi ngumu Sana kuimudu na kuona maslahi ya biashara Hiyo.                                          

2.Ubunifu bidii katika biashara ni mhimu Lakini mhimu zaidi ni uvumilivu katika faida na hasara maana kuanzisha biashara kuna mawili aidha faida au hasara usipojipanga vizuri.                                    

3.Mara nyingi mawazo mengi ya biashara hutawaliwa na dhana potofu ya kutokujiamini kuwa nianzishe biashara gani, mtaji nitapata wapi na wateja nitawapataje. Ukiamuamua kufanya achana na dhana hizo Fanya kweli.                                                              

4.Watu wengi huanzisha biashara kwa sababu ya utashi wa vitu wanavyopendelea kufanya au utaalamu walionao. Biashara za namna hii hushindwa kudumu kutokana na wahusika kutokuwa na elimu ya kuanzisha na kuendeleza biashara. Hivyo pamoja na utashi wa bisahara unayotaka kuanzisha ni mhimu ukajifunza kwanza ndipo uanzishe.                                                                                  

5.Masoko,kodi,kutangaza biashara, pamoja na mauzo ni miongoni mwa vitu mhimu Sana kuvielewa kabla ya kuamua ni biashara gani uanzishe au ununue.                                                                                       

6.Elimu bila vitendo ni kazi bure, hivyo ukijifunza na kuelewa jinsi ya kuanzisha  biashara unatakiwa uanze Mara moja ili upate uzoefu. Itakuchukua si chini ya Miezi Sita kupata uzoefu halisi kwa hiyo unatakiwa kuwa na subira.                                                                   

7.Barabara ya kuelekea katika furaha ya kweli kupitia biashara imejengeka katika kanuni kuu mbili (i)Fanya biashara inayohusisha kitu ambacho unapendelea kukifanya (II) fanya kile ambacho una uhakika unaweza kukifanya vizuri na kwa ufanisi mkubwa.               

8.Biashara mpya ni kama mtoto mchanga, inahitaji upendo, matunzo, muda pamoja na uangalifu mkubwa ili ikue katika afya bora.                                                                                                               

9.Namna nzuri ya kutambua ni vitu gani unavyopenda kuvifanya ambavyo vinaweza kuwa biashara ni kuangalia mambo unayopendelea kiasi kwamba haipiti siku bila kuyafanya. Ukishayabaini mambo hayo tafakari/waza biashara inayoendana na mambo hayo.                                                                                             

10.Pesa na utajiri vimejificha kwenye matatizo na mahitaji ya watu. Utalipwa kwa kutimiza mahitaji yao au kutatua matatizo yao. Ukitimiza mahitaji yao na kutatua matatizo yao vizuri kuliko wengine utapata pesa nyingi zaidi.

           Tumia fursa yako
           Ongeza thamani yako

                               Chief Mwinula

Sunday, 27 August 2017

FURSA

UTANGULIZI
Fursa ni nafasi ya kufanya jambo lolote lenye manufaa. (An opportunity is favourable time or set of circumstance of doing something) Chochote unachoweza kufanya na kikaleta manufaa ni FURSA.
Jambo lolote zuri huwa na manufaa pale tu mhusika anapoamua kulifanya kwa vitendo, na hii ndo maana halisi ya kutumia fursa.
Chanzo kikubw cha umaskini na kutofanikiwa katika nyanja mbalimbali kimaishi ni kutotumia vizuri fursa tulizonazo. (The big mistake in life is to let an ample opportunity lie dormant) Watu wengi wanashindwa kunufaika na fursa zao aidha kwa sababu hawazitambui au hawajui namna ya kuzitumia .

Karibu sana katika page hii tujifunze mengi juu ya na namna ya kutaua na kutumia fursa tulizonazo. 

Tuesday, 8 August 2017

ISHI KULINGANA NA FALSAFA YAKO

UNAHITAJI MAFANIKIO YA KWELI?

Mbinu zifuatazo zitakusaidia kufikia mafanikio hayo.

Kuna tofauti kubwa sana kati yakuielewa falsafa na kuiishi falsafa.Falsafa ni mawazo ambayo huonekana ya maana pale tu yanapofanyiwa kazi na matokeo yakaonekana.Usiishie kuwaza/kufikiri pekee bali tenda yale unayoyawaza ndipo yatakuwa na msaada.    (Msingi mhimu katika
maisha ni kuwaza na kutenda)

Kuna watu wengi sana ambao wanataka kutenda pasipo kuwaza na wengine wanawaza pasipo kutenda. Huyu anayetaka kutenda  bila kuwaza unaweza jiuliza anatenda nini? Pengine anaweza tenda kile alichoamriwa na mwingine, hata hivyo hatakitenda sawasawa na jinsi kinavyotakiwa kuwa na matokeo yake kufanikiwa ni kidogo. Pi mawazo bila vitedo ni bure maana hayawezi kuleta matokeo yoyote.   (Napenda mawazo mapya, napenda kufanya kazi)   

Kama unataka mafanikio ya kweli anza kwa kuwaza na kutambua ni Nyanja gani unataka mafanikio(kiimani,kimahusiano,kikazi,kiuchumi,kisiasa au kwa jambo lolote lile ulilopanga). Weka mikakati ya kuweza kufikia hiyo hatua unayoitamani na kasha anza kuifanyia kazi hiyo mikakati yako. (usifanye kwa mazoea)

Wakati wa utekelezaji unatakiwa kuchunguza na kubaini ni mkakati ipi kati ya yote ulojiwekea imeanza kuonyesha dalili njema.Ile inayoonekana kuzaa matunda ndiyo ya kukazana nayo lakini kwa ile inayolegalega huna budi kuachana nayo maana itakuchelewesha.Usilazimishe kitu kimoja kikuleletee matokeo tofauti. ( Ujinga ni kufanya kitu kile kile huku ukitegemea matokeo tofauti)

Mhimu kuzingatia:-

1)Tafuta wazo jipya

2)Tafuta mtu yeyote aliyewahi kufanya hiko ulichowaza kufanya

3)Ongeza maarifa zaidi kwa aidha kusoma vitabu au kuhudhuria semina zinazohusiana na wazo lako

4)Tafuta eneo sahihi la kutekeleza wazo lako

5)Anza utekelezaji

Chief Mwinula Chiefmwinula@gmail.com

Tumia fursa yako
Ongeza thamani yako

Sunday, 26 March 2017

UHALISIA

Kwa kila jambo lolote unalothubutu kulifanya, hakikisha una sababu angalau Tatu za kwa nini unafanya jambo hili.
Hii itakusaidia kusonga mbele na kutokata Tamaa , maana sababu ya kwanza isipoleta matokeo unayotarajia basi sababu ya pili au tatu itakuwa vizuri na kukufanya usonge mbele na hatimaye kusudi halisi litafanikiwa.
#muda pamoja na afya njema ndizo fursa pekee mhimu za kuanza nazo katika safari ya kutimiza ndoto zako#
           ANZA SAFARI SASA