Friday, 29 December 2017

KIFUNGO CHA FIKRA

TAFAKURI YA MWISHO WA MWAKA 2017

AMUA KUWA HURU KUTOKA KATIKA KIFUNGO  CHAKO

Katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania tumeshuhudia Rais na Amiri Jeshi mkuu akitumia vyema wajibu wake wa kisheria kusamehe wafungwa kwa baadhi yao kuwaachia huru na wengine kuwapunguzia vifungo vyao.
Kikubwa zaidi kilichoibua shangwe, furaha na pengine mijadala kila kona ya nchi ni kitendo  cha Raisi kusamehe Wale waliokuwa wamefungwa kifungo cha maisha pamoja na baadhi ya Wale waliohukumiwa kunyongwa.
Kitendo cha mfungwa kuachiwa huru huleta furaha kubwa Sana kwake na kwa familia yake pia. Hii hutokana na ukweli kwamba hufufua ndoto na malengo yake ambayo ni dhahiri yalianza kupotea kutokana na kuwa katikati ya kuta za gereza pasipo na matumaini ya kutoka.  Hata kama mfungwa huyo alifungwa kifungo cha muda maalumu ndoto zake huchelewa kutimia kutokana na muda anaopoteza akiwa gerezani.

Msamaha kwa mfungwa hutokana na bahati tu kwani kwani kuna wafungwa wengi walio na nafasi ya kusamehewa kutokana na vigezo husika, lakini kutokana na ufinyu wa nafasi za msamaha ndipo Bahati ikamwangukia aliyesamehewa.
      Tukiacha wafungwa walio magerezani kwa sababu ya makosa mbalimbali kutokana na sheria na taratibu za nchi ambao wanapaswa kukaa humo kwa muda fulani, maisha au pengine kusubiria kunyongwa au kubahatika msamaha, pia kuna wafungwa wengi sana katika jamii yetu ambao kisheria wako huru lakini kifikra wamezungukwa na kuta nene za gereza huru.
        Wafungwa wa namna hii wapo wengi sana lakini kwa walio wengi hawajitambui kuwa wako kifungoni kwa kiburi cha kuwa huru kisheria. Kifungo cha namna hii ni cha fikra. Fikra zimefungwa na mambo mbalimbali ambayo kiukweli yanatesa sehemu kubwa ya maisha na pengine kusababisha majuto makubwa kwa mhusika. Jambo la heri ni kwamba vifungo vya namna hii havihitaji Msamaha kutoka kwa mtu/kiongozi yeyote bali ni uamuzi wa mhusika kuamua kuwa huru baada ya kukitambua kifungo chake.
       Katika makala hii nitajaribu kukupitisha katika sehemu mbalimbali za yetu ya kila Siku ambayo ni vifungo Lakini hatuvitambui. Kama utaweza kutambua kifungo moja wapo kinahusu maisha yako, amua mara moja kuchukua uamuzi wa busara kuwa huru.
        1)MADENI# Kuna watu wapo katika kifungo cha madeni, wamekopa na wanadaiwakkila kona ya mtaa mpaka imefikia hatua wanakosa raha na kujutia. Mbaya zaidi ni kwamba pesa walizokopa hazikufanya kazi kama walivyotarjia, hivyo wamebaki wakilipa madeni kwa Majuto. Mipango yao imesimama kupisha madeni.
           2)KIPATO KUTOKIDHI MAHITAJI# mtindo huu wa maisha unawatesa watu wengi Sana, wafanyakazi serikalini, sekta binafsi na Wale wenye shughuli zao binafsi. Wanapata kipato kutokana na aidha mishahara, au kutokana na shughuli zao zingne Kama bisahara lakini kipato hiki hakikidhi mahitaji au kushindwa kutimiza malengo yao mhimu. Hiki ni kifungo kibaya kuliko vyote na ndo chanzo kikuu cha vifungo vingine kama madeni, maagano ya kishetani, sonona (msongo wa mawazo), ulevi, na kwa asilimia kubwa kinaweza kusbabisha mtu kufanya maovu kinyume na sheria hatimaye kuangukia katika kifungo halisi cha gerezani.
        3) KUTEGEMEA MISAADA# kuna watu wanaendesha maisha yao kwa kuombaomba kutoka kwa ndugu, viongozi, waajiri wao, au Jamaa zao.Maisha ya namna hii yanakufanya ushindwe kuamua msitakabali mzima wa maisha yako kwani wanaokusaidia ndio wenye maamuzi juu ya ratiba yako, muda wako, na nguvu zako pia. achana na kifungo cha namna hii badala yake wekeza muda wako, nguvu zako, pamoja na mawazo yako kwenye  mipango na ndoto zako.
        4)ULEVI NA MADAWA YA KULEVYA# kutokujizuia katika ulevi ni kifungo. Majuto yake huonekana kutokana na madhara yatokanayo na matumizi ya pombe na madawa mengine ya kulevya. MFANO: kufirisika, ajali, ulemavu uliopata kutokana na ugomvi wa kilevi, pia maelewano duni katika familia yako sababu ya ulevi. Amua sasa kuachana na kifungo hiki.
         5)MFUMO WA MAISHA UNAOENDEKEZA NI KIFUNGO KWAKO# kuna baadhi ya mifumo ya maisha isiyo na faida imewafanya baadhi ya watu kuteseka kifikra pasipo sababu ya msingi. Pengine kupitia vitu fulani ambavyo wanapenda kuvitumia ambavyo siyo mhimu lakini huwafanya wateseke wakivikosa. Mfano:- sigara, kahawa, kucheza karata, bao au hata kuangalia kipindi fulani cha televisheni. Amua sasa kupunguza ama kuachana kabisa na m
Vitu hivi na utumie muda na akili yako kukamilisha ndoto zako.
         6)MATUMIZI YA MITANDAO  YA KIJAMII# Ni dhahiri kuwa kila maendeleo huja na kasoro zake, kukua kwa teknolojia ya mawasiliano hasa ujio wa simu Za smartphone na uanzishwaji wa mitandao kama facebook, whatsapp, twitter na mingine mingi imekuwa tatizo kwa watumiaji  kwani
       Walio wengi wanapoteza muda wao mwingi kwenye mitandao kwa mambo ya ovyo kabisa. Watumiaji wa namna hii huteseka Sana kimawazo wakikosa pesa ya kununulia kifurushi cha internet. Kama nawe ni miongoni mwao,yakupasa uwe huru kwa kutumia vizuri teknolojia hii.
       🐇  NB: MICHEZO YA KUBAHATISHA NAHISI NAYO NI KIFUNGO HURU KIPYA ZAIDI  😃

Tunapofunga mwaka 2017 achana na mifumo ya maisha yako ambayo kupitia makala hii umetambua kuwa ni kifungo kwako. Achana na yale yaliyokukwamilisha kufikia malengo yako pasipo sababu za msingi.
                          "Tawala maisha yako"
              Chief Mwinula

No comments:

Post a Comment