ZAMA ZA SASA
Baada ya Zama za viwanda (industrial age) kupita sasa tupo katika zama za habari (information age). Enzi ya Zama za viwanda kulikuwa na kauli mbiu ya SOMA KWA BIDII PATA MAKISI NZURI PATA AJILI NZURI ISHI MAISHA MAZURI. Katika zama hizo mfanyakazi Pekee ndiye aliyekuwa na usalama wa maisha yake kiuchumi (job security). Lakini kauli mbiu katika zama hizi za sasa ni MWENYE HABARI SAHIHI KWA MUDA SAHIHI NDIYE ANAYEFANIKIWA. Haitoshi tu kuwa na habari sahihi ukafanikiwa bali pia yakupasa kuwa na MAARIFA SAHIHI.
Naposema maarifa sahihi simanishi uhalali wa taaluma yako, bali ni maarifa ya ziada ambayo yanaweza kuibadilisha hiyo habari sahihi na kuwa pesa. Kwa lugha nyingine hiyo habari sahihi ni FURSA.
Fursa inaweza ikawa imeenda sambamba na taaluma yako, au inaweza ikahusika na eneo unaloishi, au ikawa sawa na kazi unayofanya, na pengine ikawiana na muda wako wa ziada. Lakini ikawa ngumu kwako kuitumia kwa sababu huna maarifa ya ziada hivyo ukashindwa kunufaika nayo.
Hivyo basi katika zama hizi za habari kuna elimu ambazo hutakiwi kuzikosa hata kidogo angalau kila siku ya maisha yako kwani utaongeza maarifa ya ziada ili uweze kukabiliana vyema na fursa zinazojitokeza. Elimu hizi ni kama ifuatavyo:-
(1)ELIMU YA PESA, hii itakusaidia kuielewa pesa kwa undani zaidi inavyopatikana, inavyopaswa kutumika, inavyoweza kuongezeka na miiko yake. Kwa ujumla uelewe kanuni ya pesa, kwani wengi hushindwa kutumia fursa kwa kisingizio cha kukosa pesa.
(2)ELIMU YA BIASHARA NA UJASILIAMALI, hii itakusaidia kuelewa kanuni ya kuanza kidogokidogo kufikia mafanikio, namna ya kukuza biashara, jinsi ya kuepuka hatari katika biashara, utajifunza kanuni za mauzo na ushindani pia utajifunza uthubutu. Watu wengi wanashindwa kuanza biashara kwa kukosa maarifa ya uthubutu pia biashara nyingi hufa mapema kwa kukosa maarifa haya.
(3)ELIMU YA MAHUSIANO, hapa namaanisha uhusiano baina yako na jamii inayokuzunguka, Kama vile ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzio na kila mtu unayekutana naye haijalishi mnafahamiana au laa. Hii itakuweka karibu na kila mtu hivyo utajiongezea wigo wa kupata habari nzuri za fursa, na pengine kupata mtu mwenye uwezo wa kukupa sapoti kimawazo na kifedha pia.
(4)ELIMU YA TEKINOLOJIA NA MAWASILIANO, hii itakusaidia kupata habari mapema kupitia vyombo vya kisasa vya mawasiliano Kama vile simu na komputa kupitia internet. Pia itakurahisishia utekelezaji wa fursa zako Kama vile online marketing, electronic business(biashara mtandaoni) pamoja na kupata ujuzi zaidi wa kitu unachofanya kupitia maandiko na video za mtandaoni.
Asilimia kubwa elimu hizi hazimo kwenye mitaala ya mfumo wetu rasmi wa elimu nchini, hata Kama baadhi zipo lakini si katika mkitadha wa kile ninachokimaanisha cha ulazima wa kila apendaye mafanikio ajifunze maarifa haya haijalishi ana taaluma gani.
Maarifa haya unaweza kuyapata kwa kusoma vitabu kuhudhuria semina, kusikiliza mafundisho kwa njia ya sauti(audio) au video mtandaoni pia kwa kupata ushauri na uzoefu kwa wale walioanza zamani kuyaishi maarifa haya.
NB, ukishayapata maarifa haya, anza kuyafanyia kazi Mara moja ndipo utakapoona ilivyo rahisi kufanikiwa katika Zama hizi za habari.
ASANTE
Tumia fursa yako
Chief Mwinula
Sunday, 14 January 2018
ZAMA ZA HABARI
Subscribe to:
Posts (Atom)