Thursday, 15 February 2018

NAPENDA BIASHARA

BIASHARA NZURI KUFANYA KWA MWAKA 2018

Kutokana na serikali kubana matumizi na kusababisha pesa kupungua katika mzunguko, watu wengi hususani Wenye mitaji midogo wamebaki hawajui ni biashara gani wafanye yenye kuhitaji mtaji kidogo lakini iwe na faida nzuri.
        Hali hii imekuwa kikwazo kwa wengi wanaotamani kuanzisha biashara hasa wale wasiofuatilia mafunzo ya biashara na ujasirimali na elimu ya fedha kwa ujumla.
         Leo nitakushirikisha kwa ufupi biashara chache na uwekezaji unaoweza kufanya kipindi hiki cha uadimu wa pesa.
          Zifuatazo ni biashara tatu zinazohitaji mtaji kidogo lakini zinafaida kubwa kwa sana:-
 
     1)Biashara yya kuuza chakula (mgahawa). Hata Kama pesa imekuwa adimu vipi watu lazima wale, jaribu kufanya utafiti aina ya chakula kinachohitajika sana katika eneo lako kisha anza biashara hiyo mara moja.

        (2)Kilimo cha kibiashara. Kilimo hiki kinahusisha mazao pendwa ambayo hukomaa ndani ya muda mfupi hasa mazao ya bustani na matunda.
   
        (3)Ufugaji wa kibiashara. Ufugaji huu unahusisha wanyama Kama sungura, ng'ombe wa maziwa pamoja na kuku.

        Uwekezaji ambao unaweza kufanya usiohitaji muda wako mwingi kuusimamia.
        
           (1)Uwekezaji katika mfuko wa umoja wa UTT, tembelea ofisi zao kupata maelezo mhimu.
            (2)Kununua hisa katika soko la hisa.  hapa unatakiwa uwe unafuatilia kwa makini ili kujua soko la hisa likoje na kampuni gani hisa zake zinauzika kirahisi kwa faida.
             (3)Biashara ya mtandao (network marketing).Biashara hii inahitaji umakini na elimu ya kutosha juu ya biashara hii, nakushauri upate kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO kilichoandikwa na Amani makrita, Tsh 5000 unapata soft copy wasiliane naye kwa namba 0755953887
             (4)Uwekezaji katika viwanja. Nunua kiwanja na kiache tu baada ya muda utauza kwa faida.
           (5)Wekeza katika majengo. Kama una mtaji wa kutosha jenga nyumba aidha ya kuishi au kibiashara halafu pangisha.

MHIMU:- Kuna changamoto kubwa ya baadhi ya watu kuwa na mtaji lakini wanashindwa kuanza biashara kwa sababu ya kukosa muda wa kusimamia biashara hizo. Suluhu ya changamoto hii ni kutafuta MSHIRIKA.
        Mshirika wako katika biashara si mfanyakazi wako bali ni mtu ambaye kwa pamoja mnamiliki biashara hiyo.

    Faida ya kuwa na mshirika
(1)Ataweza kufuatilia mambo mhimu ya biashara ambayo wewe huwezi kufuatilia kutokana na kubanwa na kazi.
(2)Kama kazi yako hairuhusu kuwa na biashara unaweza kuanza biashara kwa njia hii.

       Mambo ya kuzingatia kwa mtu unaye mchagua kuwa mshirika wako.
(1)Uaminifu
(2)Kujituma kwenye kazi
(3)Awe na malengo na nidhamu ya fedha
(4)Asiwe na tabia hatarishi Kama ulevi na starehe.
(5)Awe na uelewa juu ya biashara mnayo taka kufanya.

     
                            Chief Mwinula