Sunday, 24 September 2017

BIASHARA

ANZISHA BIASHARA YAKO SASA

            sehemu ya kwanza

1.Kuanzisha biashara ni moja ya maamuzi mazuri na sahihi katika maisha. Lakini ukianza bila Elimu ya kutosha juu ya biashara hiyo itakuwa kazi ngumu Sana kuimudu na kuona maslahi ya biashara Hiyo.                                          

2.Ubunifu bidii katika biashara ni mhimu Lakini mhimu zaidi ni uvumilivu katika faida na hasara maana kuanzisha biashara kuna mawili aidha faida au hasara usipojipanga vizuri.                                    

3.Mara nyingi mawazo mengi ya biashara hutawaliwa na dhana potofu ya kutokujiamini kuwa nianzishe biashara gani, mtaji nitapata wapi na wateja nitawapataje. Ukiamuamua kufanya achana na dhana hizo Fanya kweli.                                                              

4.Watu wengi huanzisha biashara kwa sababu ya utashi wa vitu wanavyopendelea kufanya au utaalamu walionao. Biashara za namna hii hushindwa kudumu kutokana na wahusika kutokuwa na elimu ya kuanzisha na kuendeleza biashara. Hivyo pamoja na utashi wa bisahara unayotaka kuanzisha ni mhimu ukajifunza kwanza ndipo uanzishe.                                                                                  

5.Masoko,kodi,kutangaza biashara, pamoja na mauzo ni miongoni mwa vitu mhimu Sana kuvielewa kabla ya kuamua ni biashara gani uanzishe au ununue.                                                                                       

6.Elimu bila vitendo ni kazi bure, hivyo ukijifunza na kuelewa jinsi ya kuanzisha  biashara unatakiwa uanze Mara moja ili upate uzoefu. Itakuchukua si chini ya Miezi Sita kupata uzoefu halisi kwa hiyo unatakiwa kuwa na subira.                                                                   

7.Barabara ya kuelekea katika furaha ya kweli kupitia biashara imejengeka katika kanuni kuu mbili (i)Fanya biashara inayohusisha kitu ambacho unapendelea kukifanya (II) fanya kile ambacho una uhakika unaweza kukifanya vizuri na kwa ufanisi mkubwa.               

8.Biashara mpya ni kama mtoto mchanga, inahitaji upendo, matunzo, muda pamoja na uangalifu mkubwa ili ikue katika afya bora.                                                                                                               

9.Namna nzuri ya kutambua ni vitu gani unavyopenda kuvifanya ambavyo vinaweza kuwa biashara ni kuangalia mambo unayopendelea kiasi kwamba haipiti siku bila kuyafanya. Ukishayabaini mambo hayo tafakari/waza biashara inayoendana na mambo hayo.                                                                                             

10.Pesa na utajiri vimejificha kwenye matatizo na mahitaji ya watu. Utalipwa kwa kutimiza mahitaji yao au kutatua matatizo yao. Ukitimiza mahitaji yao na kutatua matatizo yao vizuri kuliko wengine utapata pesa nyingi zaidi.

           Tumia fursa yako
           Ongeza thamani yako

                               Chief Mwinula

No comments:

Post a Comment